Leo May 23, 2018 Askofu Mkuu wa kanisa katoliki nchiniAustralia, Adelaide Philip Wilson amejiuzulu nafasi yake ya uongozi wa juu wa kanisa hilo baada ya kukutwa na hatia ya kuficha uovu uliotendwa na Padri mwezake Fletcher wa kulawiti.
Askofu huyo mwenye miaka 67 anakabiliwa na kifungo cha miaka 2 jela kwa kosa hilo la kufumbia macho na kushindwa kutoa ripoti kwa mamlaka husika juu ya kitendo hicho ambacho ni kinyume na sheria za nchini humo alichokifanya Padre James Fletcher cha kulawiti watoto wanaotumikia kanisani kwenye miaka 1970.
Wilson ambaye ndiye Askofu mwenye nafasi juu ya uongozi wa kanisa Katoliki Australia amesema anaachia madaraka yake ya uongozi wa kanisa hilo na yuko tayari hata kujiuzulu uaskofu wake ikimbidi kufanya hivyo.
Askofu Wilson alikuwa Padre tu wakati Padre Fletcherakifanya maovu hayo na Padre Fletcher alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela ambapo mwaka 2006 alifariki gerezani ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya hukumu.
____________________________________________________________________ ASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************* Je? Wewe ni msanii au mfanya biashara Je? Wahitaji tangazo au mziki wako uwafikie watu weng Tangaza mziki biashar tangazo NK. hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com
0 Maoni
King seven tz