Ticker

6/recent/ticker-posts

Maneno ya Rais Magufuli baada ya kupata taarifa za msiba wa Mapacha walioungangana


Maneno ya Rais Magufuli baada ya kupata taarifa za msiba wa Mapacha walioungangan


Leo June 3, 2018 Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam January 6, 2018.
Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake.
Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.
Maria na Consolata walikuwa watoto yatima, na walikuwa wakilelewa na kusomeshwa na Masista wa Maria Consolata wa Kanisa Katoliki.

____________________________________________________________________ ASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************* Je? Wewe ni msanii au mfanya biashara Je? Wahitaji tangazo au mziki wako uwafikie watu weng Tangaza mziki biashar tangazo NK. hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com

Chapisha Maoni

0 Maoni