Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepewa heshima ya kuwasha umeme katika vijiji vitatu ambavyo huduma ya kupeleka umeme imekamilika.
Zoezi hilo lilifanyika kwa nyakati tofauti, Machi 15 hadi 18 Mwaka huu, wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta za nishati na madini katika Mikoa kadhaa nchini.
Vijiji vilivyowashiwa umeme ni Nyabange kilichopo Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Kijiji cha Idala wilayani Nzega pamoja na Kijiji cha Kisaki kilichopo Mkoa wa Singida.
Akitoa ufafanuzi kwa Kamati husika, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisema kwamba, Vijiji hivyo vimepata huduma ya umeme kupitia mpango wa upelekaji umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mradi mkubwa wa umeme wa Backbone.
Tangaza biashara yako mziki matangazo yeyote upate kuwafikia watu weng zaid wasiliana nasi 0757136484 Gmail. Kingsevenmedia@gmail.com
0 Maoni
King seven tz