Kuelekea tamasha la mkesha wa Pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi mwaka huu,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo linalotarajia kufanyika jiji Mwanza.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mwenyekitiki wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maadalizi kuelekea siku hiyo yamekamilika na Waziri Nchemba amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo linalotarajia kuwashirikisha waimbaji 16 wa Kitaifa na kimataifa.
''Awali tulitarajia mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu lakini imeshindikana kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi ya kikazi hivyo Nchemba atamwakilisha katika uzinduzi wa tamasha hilo" amesema Msama.
Msama pia aliwataja baadhi ya viongozi watakaokuwepo kwenye tamasha hilo, Nibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angela Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na kamanda wa Polisi wa Mwanza, Ahmed Msangi.
Aliongeza kuwa mandalizi yanaendelea vizuri kabisa, tumejipanga ili kuhakikisha kila tulichokikusudia kitafanyika kwa mwaka huu, ulinzi wa kutosha pia kutakuwa na viongozi wa dini, Serikali pamoja na taasisi mbalimbali.
Baadhi ya waimbaji waliothibitisha kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya uimbaji kuwa ni pamoja na malkia wa muziki wa Injili nchini, Rose Mhando ambae yeye atazindua albamu yake mpya, wengine ni Ephram Sekeleti, Angel Benard, Paul Clemen, Bonny Mwaitege, Jesca Honore, Betrice Mwaipaja, Christian Shusho, Christopher Muhangila na Upendo Nkone.
Msama alimalizia kuwa kwa kubainisha viingilio vya vya tamasha hilo Mwanza
itakua ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watotoni shilingi 2000, wakati Simiyu wakubwa watatoa shilingi 3000 na watoto shilingi 2000.
Mwenyekiti huyo mbali na kutaja viingilio hivyo pia alitoa wito kwa wakazi wa kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kuja kushughudia Baraka za Mungu kwani waimbaji wamejiandaa kuimba kwa kutumia vyombo.
''Awali tulitarajia mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu lakini imeshindikana kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi ya kikazi hivyo Nchemba atamwakilisha katika uzinduzi wa tamasha hilo" amesema Msama.
Msama pia aliwataja baadhi ya viongozi watakaokuwepo kwenye tamasha hilo, Nibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angela Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na kamanda wa Polisi wa Mwanza, Ahmed Msangi.
Aliongeza kuwa mandalizi yanaendelea vizuri kabisa, tumejipanga ili kuhakikisha kila tulichokikusudia kitafanyika kwa mwaka huu, ulinzi wa kutosha pia kutakuwa na viongozi wa dini, Serikali pamoja na taasisi mbalimbali.
Baadhi ya waimbaji waliothibitisha kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya uimbaji kuwa ni pamoja na malkia wa muziki wa Injili nchini, Rose Mhando ambae yeye atazindua albamu yake mpya, wengine ni Ephram Sekeleti, Angel Benard, Paul Clemen, Bonny Mwaitege, Jesca Honore, Betrice Mwaipaja, Christian Shusho, Christopher Muhangila na Upendo Nkone.
Msama alimalizia kuwa kwa kubainisha viingilio vya vya tamasha hilo Mwanza
itakua ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watotoni shilingi 2000, wakati Simiyu wakubwa watatoa shilingi 3000 na watoto shilingi 2000.
0 Maoni
King seven tz