Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amepongeza ahadi ya Korea kaskazini kusimamisha majaribio yake ya kinyuklia na ufyatuaji wa makombora huku akitoa angalizo kuwa Tokyo itaendelea kuishinikiza zaidi serikali ya Pyongyang.
Abe amesema hatua hiyo inatia matumaini lakini cha muhimu ni utekelezwaji kufanyika kwa ukweli na kwa namna inayokubalika.
Hayo yanajiri baada ya Kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un jumamosi hii kuahidi kwamba taifa lake litasimamisha majaribio yake ya kinyuklia hatua iliyopongezwa na Marekani na Korea Kusini.
Tamko hilo la Korea Kaskazini linakuwa hatua muhimu katika kutatua mzozo wa kidiplomasia kati ya Korea Kaskazini na mataifa ya magharibi.
Hatua hii inakuja katika kipindi kisichozidi juma moja kabla ya kiongozi wa Korea Kaskazini kukutana na wa kusini Moon Jae-in kwa ajili ya mazungumzo ya kuharibu silaha za nyuklia kuelekea mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati yake na raisi wa Marekani Donald Trump

____________________________________________________________________ ASASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************"""** Tangaza biashara mziki Nk. yako hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com
0 Maoni
King seven tz