Miili ya pacha walioungana Maria na Consolata iliwasili kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha Iringa (Rucu) kwaajili ya kuagwa Jana.
Tukio la kuagwa kwa pacha hao limetangazwa kuwa ni la kitaifa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ameeleza kuwa Rais John Magufuli ni miongoni mwa walioguswa na kuhuzunishwa na vifo hivyo.
"Huu ni msiba wa kitaifa Rais angehudhuria ila amebanwa na ratiba Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Sera, Bunge na Walemavu, Stella Ikupa wataudhuria hapa," amesema Kasesela.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru ni miongoni mwa watu waliohudhuria akaeleza kusikitishwa na vifo hivyo kwa kuwa vimezuia pacha hao kutotimiza ndoto zao za kuwa wanataaluma.
Anatumia nafasi Hiyo kuwasihi wanafunzi kutambua mikopo inayotolewa ni rasilimali muhimu, Serikali inalenga kuwawezesha ili wawe wataalam watakaosaidia nchi.
____________________________________________________________________ ASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************* Je? Wewe ni msanii au mfanya biashara Je? Wahitaji tangazo au mziki wako uwafikie watu weng Tangaza mziki biashar tangazo NK. hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com
0 Maoni
King seven tz