Miaka michache iliyopita nilipata bahati kufanya kazi katika kampuni fulani, ili kutokana na wadhifa wa kampuni hiyo naomba kampuni hiyo niiwekee (pattern). Nilifanya kazi kwa moyo mkunjufu pasipo kuionea haya kazi hiyo.
Juhudi, nguvu , bidii na utashi alionijalia MMungu ndiyo ulikuwa umeitawala nafsi na akili yangu katika kufanya kazi ile, yapo mengi ambayo nilijifunza katika kazi ile ila kwa sababu ya muda naomba nifupishe hadithi hii nitakusimulia wakati mwingine nikiwa na muda wa kutosha.
Kwa kifupi ni kwamba Kuna kipindi fulani kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu katika kuzielezea hapa siku ya leo, ni kwamba nilisimamishwa kazini hivyo niliona kama vile kila kitu kwangu kama kimesimama, kumbe ukweli haupo hivyo hata chembe.
Baada ya muda mchache kupita tangu tukio hilo litokee nilituliza akili yangu nakukubaliana na hali ambayo imetokea, japo kuna watu walinong`ona na kuziruhusu ndimi za midomo yao iweze kuyajadili maisha yangu pasipo kunishirikisha mhusika.
Wapo waliosema ya kwamba nimepotea, wengine walisema amezoea huyu wacha dunia imfundishe na maneno mengi yasiyokuwa na vichwa wala miguu naweza nikaita hivyo kwa sasa. Lakini pia katika hali ambayo ilinitokea ya kufukuzwa kazi ilinifanya niweze kujua ni yupi rafiki wa kweli na ni yupi lakini muongo.
Kwa kifupi ni kwamba maisha ya kufukuzwa kazi yapo kama yalinipata mimi na nikaweza kuinuka upya najua hata kwako inawezekana cha msingi ninachotaka kukwambia ni kwamba
Zipo alama ambazo umewekewa na jamii yako inayokuzunguka na alama hizo kuna wakati zinakupoteza sana. Kwa mfano, umeambiwa na kuwekewa alama kwamba wewe ni mjinga, huwezi kitu, ni maskini na pengine hufai.
Lakini katika uhalisia ulivyo, wewe hauko hivyo kama jamii ilivyokupachika alama hizo. Wewe ni mtu wa mafanikio ikiwa utalielewa hilo na kuchukua hatua sitahiki ambazo zinaweza kubadilisha maisha yako na kufutilia mbali alama hizo, hajarishi umefukuzwa kazi jua ya kwamba kuna maisha mengine nje ya ajira na mafanikio yako yapo palepale.
Usijaribu kuamini kila ambacho unaambiwa na watu wengine, ikiwa utaamini hizo alama ambazo unapewa na jamii yako tambua hutaweza kufanya kitu chochote. Utabaki hapo ulipo na kuumia sana, jambo la msingi unalotakiwa kuamini ya kwamba wewe ni mshindi na kila kitu ambacho hutokea katika maisha ya mwanadamu hutokea kwa sababu maalumu, hivyo jifunze kwa kila kitu kinachotea katika maisha yako kwani kila kitu kina funzo ndani yake.
Asante nikutakie siku njema na mafanikio mema pia

______________________________________________________________________ ASASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************"""** Tangaza biashara mziki Nk. yako hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com
0 Maoni
King seven tz