Ticker

6/recent/ticker-posts

Nandy na Bill Nas waibuka na hili



Msanii Bill Nas ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Tagi ubavu' amefunguka na kusema kuwa kuna kazi ambayo amefanya na msanii Nandy na kudai kuwa anaamini wimbo huo utatoka wakati ukifika.

Bill Nas ameweka wazi hayo leo Mei 2, 2018 akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV na kudai kuwa yeye na Nandy sasa wanaendelea kuishi kama marafiki na kuwa upo wimbo wamefanya pamoja.

"Kuna wimbo tumefanya pamoja, wimbo umefanywa chini ya S2KIZZY hivyo naamini muda ukifika utatoka tu ila nachojua ni wimbo mkali, kuhusu jambo ambalo limetokea kuhusu mimi na yeye tayari nilishaomba radhi kwa wananchi na sasa maisha ya kawaida yanaendelea, hivyo hatuna tofauti yoyote ile kwa kuwa yule ni rafiki yangu na nina iheshimu sana familia yake akiwa pamoja na mama yake kwa kuwa ni mtu ambaye amekuwa akijitoa sana ku-support kazi za mwanaye" alisema Bill Nas

Mbali na hilo Bill Nas amedai kuwa katika wasanii wa kike wawili ambao wanafanya vizuri nasi Vanessa Mdee pamoja na Nandy ndiyo wasanii wanaofanya vyema kwa sasa




____________________________________________________________________ ASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************* Je? Wewe ni msanii au mfanya biashara Je? Wahitaji tangazo au mziki wako uwafikie watu weng Tangaza mziki biashar tangazo NK. hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com

Chapisha Maoni

0 Maoni