Ugonjwa wa Mabusha kuwapeleka watu mahakamani




Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewatahazarisha wananchi wa Tanzania kiujumla kuachana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanaume wenye mabusha kwa 'kuwajambisha' ama kuwapigia miruzi kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi wakati akifanya mahojiano na eatv.tv baada ya kushamiri kwa matukio mengi ya udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia licha baadhi ya watu kutofahamu kuwa wakifanya ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Vipo vifungu vya sheria vinavyoweza kumfikisha mtuhumiwa wa kitendo hicho Mahakamani pamoja kutozwa faini kulingana na mfungua mashtaka atakavyokuwa anataka kulipwa fidia kutokana na udhalilishaji aliyofanyiwa", amesema Kamanda Msangi.



____________________________________________________________________ ASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************* Je? Wewe ni msanii au mfanya biashara Je? Wahitaji tangazo au mziki wako uwafikie watu weng Tangaza mziki biashar tangazo NK. hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com

Chapisha Maoni

0 Maoni