Hospitali ya wilaya ya Manyoni inakabiliwa na upungufu wa mashuka hadi kufikia hatua ya wagonjwa kusubiri mashuka yaliyofuliwa yakauke na kutandikwa kwenye vitanda .
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni Daktari Ania Mlewa amesema hayo wakati akipokea vifaa tiba kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji wa mtaa wa Samaria Bwana Moses Ntandu na kusema kuwa wodi ya wazazi ya akina mama ndiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa.
Akikabidhi vifaa tiba ambavyo ni mashuka tisini,vifaa vya kujifungulia pamoja na kitanda chake,vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni saba na laki nne,mdau wa afya ambaye pia ni wa kitongoji cha samaria bwana moses ntandu ,amesema zoezi hilo ni kuunga mkono juhudi za Mheshimwa rais katika kuhakikisha shekta ya afya ina kuwa na vifaa tiba,baada ya kuona upungufu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni na kuandika andiko kwa rafiki yake Uingereza na kupata msaada huo.
Akipokea na kuvikabidhi wa uongozi wa hospitali Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni Bwana Moses Matonya,amewataka wananchi kutumia elimu walizozipata hapa nchini,kuandika maandiko ambayo yatalenga kusaidia sekta mbalimbali za kijamii zinazokabiliwa na matatizo.
____________________________________________________________________ ASANTE KWA KUFUNGUA POST HII Tuna kusihii endelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza meng pia kwa kupakua nyimbo mpya kila Siku ********************************************************* Je? Wewe ni msanii au mfanya biashara Je? Wahitaji tangazo au mziki wako uwafikie watu weng Tangaza mziki biashar tangazo NK. hapa wasiliana nasi 0757136484 Email. Kingsevenmedia@gmail.com
0 Maoni
King seven tz